SERIKALI YA MAMA SAMIA YARUHUSU MIKUTANO YA HADHARA

 

RAIS Dkt. SAMIA ARUHUSU MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA

Posted On: January 5/2023

KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza maamuzi ya serikali ya  kuondoa zuio la vyama vya Siasa kufanya mikutano ya hadhara.

Aidha mheshimiwa Rais amevitaka vyama vya Siasa kutumia mikutano ya hadhara  kuikosoa na kuishauri serikali kistaarabu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Rais ametangaza maamuzi hayo wakati akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa, Ikulu Jijini Dar es salaam na kuweka wazi kuwa serikali imedhamiria kukwamua mchakato wa kupata katiba mpya baada ya kukaa na kukubaliana na vyama vya siasa.

Aidha amebainisha kuwa mchakato huo wa katiba mpya utategemea hali ya nchi, uwezo wa kiuchumi, pamoja na mila na desturi.

Wakati huo huo Rais Samia amesema Serikali inajiandaa kurekebisha sheria anuai zikiwemo Sheria za Uchaguzi na sheria za vyama vya siasa ili kujenga Taifa lenye umojai

Mheshimiwa Rais ameongeza kuwa ili Taifa liwe na umoja lazima kuwe na maridhiano baina ya vyama vya siasa kwa lengo la kuendesha Taifa lenye amani na utulivu kwa maendeleo ya Taifa letu.

KaziInaendelea


Post a Comment

0 Comments